Imaam Ibn Baaz - Hukmu Ya Anayeswali Ijumaa Pekee Na Kuacha Swalaah Zilizobaki

SWALI: Kuna mtu anaswali Ijumaa pekee bila kuswali Fardhi zilizobaki, je, inakubaliwa Swalaah yake?

JIBU: Haikubaliwi Swalaah yake, kwa hakika amekuwa Kafiri kwa hilo. Swalaah yake ya Ijumaa, Swawm yake, na matendo yake yote ni batili. Anasema Aliyetukuka: "Na kama wangemshirikisha bila shaka yangebatilika yale waliyokuwa wakitenda." [Al-An'aam: 88] Na Anasema Aliyetakasika: "Na yeyote atakayekufuru iymaan; basi kwa yakini zimebatilika 'amali zake; naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika." [Al-Maaidah: 5] Basi yule anayekufuru kufru kubwa au shirki kubwa, huporomoka matendo yake. Tunamuomba Allaah afya (Atulinde). Na kuacha Swalaah ni kufru kubwa." [Nuwr 'Alaa Ad-Darb, 13/339]

Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
NAMNA YA SWALAH YA IJUMAA