Imaam Ibn #039;Uthaymiyn: Kusikiliza Nyimbo Baada Ya Swalaah; Je, Swalaah Itakubaliwa?

SWALI: Baadhi ya nyakati huwa nasikiliza nyimbo baada ya Swalaah. Mfano huenda kuswali kisha nnapoingia garini husikiliza nyimbo. Je Swalaah yangu itakubaliwa?

JIBU: Ama kuhusu Swalaah yako ni sahihi. Lakini kusikiliza nyimbo ni haramu. Kwa hiyo inakuwajibika kuacha ee ndugu! Bali ni bora kwako usikilize Qur-aan au khabari (redioni) ili uokoke na madhambi haya. [Fataawa Kuhusu Swalaah]
Vitambulisho: