Imaam Ibn Baaz - Hukmu Ya Kucheka Ndani Ya Swalaah

SWALI: Ni nini hukmu ya kucheka ndani ya Swalaah, na je, anayecheka katika Swalaah, anapaswa kurudia?

dani ya Swalaah kunaivunja Swalaah kwa makubaliano ya Wanachuoni. Anapocheka ndani ya Swalaah, imebatilika. Na hivyo pia kwa atakayezungumza ndani ya Swalaah kwa makusudi, hubatilika Swalaah yake. Isipokuwa ikiwa atakuwa amesahau au ni mjinga (asiyejua), basi hapo haitobatilika Swalaah ya mwenye kusahau na mjinga. Lakini kicheko kinabatilisha moja kwa moja, kwa sababu ni kutoipa Swalaah uzito na pia kuizembea. [Majmuw’ Al-Fataawa, juz. 29, uk. 344]




Vitambulisho: