Twahara na Aina za Maji

20869

 

Maana ya twahara

Utwahara kilugha

Kujisafisha na kujitakasa na uchafu

twahara kisheria

twahara kutokana na hadathi -Kujitwahirisha na najisi

Vigawanyo vya utwahara

1. Twahara wa ndani

Nao ni kuusafisha moyo na ushirikina na maasia na kila chenye kuutia doa. Haiwezekani kuhakikishika utwahara iwapo kutakuwa na uchafu wa ushirikina ndani ya moyo, kama ilivyo katika maana ya maneno ya Mwenyezi Mungu U:{Enyi Mlioamini! Hakika washirikina ni najisi, basi na wasiukaribie Msikiti wa Haram (Msikiti wa Makka) baada ya mwaka wao huu. Na mkiwa mnaogopa umasikini, basi Mwenyezi Mungu Atawakwasisha nyinyi kwa fadhla Zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi Mwenye hekima} [8: 28]

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) alisema: “Muumini hanajisiki.” [ Imepokewa na Bukhari na Muslim]

2.Twahara wa Nje

Nao ni twahara wa mwili kutokana na hadathi na najisi.

Na inagawanyika vigawanyiko viwili:

1.Utwahara kutokana na hadathi (hali ya kutokuwa na udhu na kuwa na janaba)

Hadathi ni kile kinachotukia katika mwili kikamzuia Mwislamu kufanya ibada ambazo zinahitaji utwahara, kama kuswali, kutufu kwenye Alkaba na zinginezo. Na inagawanyika vigawanyo viwili:

Hadathi Ndogo

Ni ile inayopasisha kutawadha kama vile kukojoa, kwenda haja kubwa na vitanguaji udhu vingine. Kujitwahirisha kwake kunakuwa kwa kutawadha. Mwenyezi Mungu U Anasema: {Enyi mlioamini! Mkiinuka kutaka kuswali, osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpanguse vichwa vyenu na mwoshe miguu yenu mpaka vifundoni} (5: 6)

Hadathi Kubwa

Hiyo ni ile inayopasisha kuoga kama vile janaba, hedhi na vinginevyo. Na kujitwahirisha nayo inakuwa kwa kuoga. Mwenyezi Mungu U Anasema i: {Na mkiwa na janaba, jitwahirisheni} (5: 6)

Hadathi inazuiya kuswali
Kutawadha ni kujitwahirisha na hadathi ndogo

2. Kujitwahirisha na Najisi:

Nao ni kuiyondoa najisi mwilini na nguoni na sehemu ya kufanya ibada, Na kuondoa najisi ni lazima kwa neno la Mwenyezi Mungu U: {Na nguo zako zitwahirishe} (74: 4)

na neno lake Mtume (s.a.w) [Mmoja wenu akija msikitini na atazame, akiona uchafu au kitu cha kuudhi kwenye viatu vyake basi na avipanguse kisha aswali navyo]
Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Ghuslu - Twahara Najisi

twahara wa mwili
twahara wa mahali
twahara wa nguo

Vigawanyo vya maji

Kwanza: Maji Yenye kutwahirisha

1. Maji ya Kawaida:

Nayo ni maji ambayo yamebaki katika sifa yaliyoumbiwa nayo, kama maji yanayoteremka kutoka mawinguni, kama vile mvua, theluji na mvua ya barafu [ Barad (barafu) ni maji makavu yanayoteremka yakiwa vipande vidogovidogo.], au yenye kutembea ardhini, kama maji ya bahari, mito na maji ya mvua na maji ya visima. Mwenyezi Mungu U Anasema: {Na tumeyateremsha kutoka mbinguni maji safi }(25: 48)

Mwenyezi Mungu U Amesema: {Na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni ili kukusafisheni kwayo} [8: 11]

Na mtume ﷺ alikuwa akiomba na kusema (Ewe Mola wangu! Nitakase na makosa yangu kwa theluji, maji na barafu) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim].

Na alisema tena ﷺ kuhusu maji ya bahari maji yake ni yenye kutwahirisha na mfu wake ni halali) [ Imepokewa na Ahmad na Abu Daud.].

Visima
Mvua
Mito
Bahari

2.Maji yaliyotumiwa:

Nayo ni maji yanayotiririka kutoka kwenye viungo vya mwenye kutawadha au mwenye kuoga. Hayo si makosa kuyatumia kujitwahirishia, kwa kuwa ilithubutu kutoka kwa Ibn Abbas t kuwa alisema kuwa mmoja katika wake wa Mtume (s.a.w) alioga kwenye chombo, na Mtume wa Mwenyezi Mungu U akataka kutawadha kutoka kwenye chombo hicho. Yule mkewe akasema: «Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi nilikuwa na janaba.” Akasema: (Maji hayaathiriki na Janaba) [ Imepokewa na Tirmidhi.].

3. Maji Yaliyochanganyika na kitu Twahara:

Nayo ni maji yaliyochanganyika na kitu twahara kama majani ya mti au mchanga au kutu kwenye matanki ya maji na kisiache athari kwenye yale maji yenye kuyafanya yasiitwe maji ya kawaida. Kwa kauli ya mtume (s.a.w) kuwaambia wanawake waliosimama kumshughulikia binti yake aliyekuwa amekufa(nae ni bi ruqiya): (Mwosheni mara tatu au nne au zaidi ya hizo kama itahitajika, kwa maji na majani ya mkunazi, na mwishoni mwake kafuri) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Maji yaliyochanganyika na mchanga
Kutu za matanki ya maji
Maji yaliyochanganyika na majani ya mti
Kugeuka kwa Maji
Maji yakigeuka kwa kitu kilichoathiri na kuyatoa kwenye jina la maji na kuyapa jina lingine kama chai au maji ya tamu (juice) na visivyokuwa hivyo, basi haisihi kujitwahirisha nayo, kwa kuwa hayaitwi maji tena.
Mchuzi
Wino
maji ya tamu, (juice)
Chai

4. Maji yaliyochanganyika na najisi na isiyabadilishe:

Nayo ni yale ambayo yaliingia ndani yake najisi, kama mkojo au mfu na vinginevyo na isibadilishe sifa zake zozote.hukmu ya Maji haya ni yenye kutwahirisha, kwa kauli ya Mtume (s.a.w) juu ya kisima cha Budhaah (Hakika maji yanatwahirisha hakuna kitu cha kuyafanya najisi) [ Imepokewa na Ahmad na Tirmidhi].

Maana yake: Watu walikuwa wakitupa uchafu pambizoni mwa kisima, na mvua ilikuwa ikiusukuma kwenye kisima.Na maji yalikuwa, kwa kuwa ni mengi, hayaathiriwi na kuingiliwa na vitu hivyo na wala hayabadiliki.

Pili: Maji Najisi

Nayo ni maji yaliyoingia ndani yake kitu chochote cha najisi kama mkojo na mfu, kikabadilisha mojawapo ya sifa tatu za hayo maji: harufu yake, tamu yake au rangi yake. Maji haya ni najisi kulingana na maoni ya wanavyuoni kwa umoja wao, na haifai kuyatumia.

Mfu usiobadilisha maji
Mfu aliebadilisha maji
Maelezo

1.Asili ya maji ni utwahara. Kukiwa na maji yasiyojulikana kama ni najisi au ni twahara, basi yatazingatiwa ni twahara kulingana na asili yake, na haifai kujilazimisha, na kujitia wasiwasi.

2.Inafaa kutawadhia maji ya Zamzam, kwa kuwa imethubutu kutoka kwa Mtume (s.a.w) aliitisha ndoo ya maji ya Zamzam akanywa kutoka kwenye hiyo ndoo na akatawadhia.