Mambo mazuri ambayo Mwenyezi Mungu aliwaumbia watu nayo, ni ambayo yanamfanya mtu akamilike mpaka afikie daraja ya sifa bora na pambo zuri.
Imepokewa kutoka kwa Aishah t kuwa alisema kwamba Mtume ﷺ alisema: (Mambo matano ni katika sifa za kimaumbile: kupunguza masharubu, kufuga ndevu, kupiga mswaki, kupuliza maji, kukata kucha, kusafisha makunjo viungoni, kusumua nywele za makapwa kunyoa nywele sehemu za siri, na kutamba kwa maji na kusukutua) [Imepokewa na Muslim.].
Ni kipande cha mti wa mpilipili – au mfano wake- kinachotumiwa kusafisha meno na chakula kilichogandamana na kuondosha harufu mbaya
Na Kupiga mswaki kumesuniwa nyakati zote, kwa kauli ya Mtume ﷺ: (Kupiga mswaki kunatwahirisha kinywa, kunamridhisha Mola) [Imepokewa na Ahmad].
Lakini imetiliwa mkazo kupiga mswaki katika sehemu zifuatazo: -
1. wakati wa kutawadha
Kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Lau si kwa kuwaonea uzito umma wangu ningaliwaamrisha kupiga mswaki kila wanapotawadha) [Imepokewa na Ahmad].
2. Wakati wa kuswali
Kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Lau si kwa kuwaonea uzito umma wangu ningaliwaamrisha kupiga mswaki kila wanapotaka kuswali) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
3. Wakati wa kuingia nyumbani
Imepokewa kwa al- Miqdad kumpokea babake t alisema: (Nilimuuliza Aishah t kuhusu kitu ambacho Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akikianzia akiingia nyumbani kwake. Akasema “Mswaki” [Imepokewa na Muslim.].
4. Wakati wa kuamka kutoka usingizini
Amepokewa Hudhaifah (RA) akisema: Mtume ﷺ alikuwa akiinuka usiku akisafisha kinywa chake kw a mswaki) [Imepokewa na Bukhari.].
5. Wakati wa kusoma Qur›ani:
Alipokewa Ali t akiamuru mswaki na akasema kwamba Mtume ﷺ alisema: (Hakika mja akipiga mswaki, kisha akasimama kuswali, Malika husimama nyuma yake akisikiliza kisomo chake, na humkaribia- au neno mfano wa hilo- mpaka kuweka kinywa chake juu ya kinywa yule, ikawa hakuna chochote cha qur’ani kitokacho kwake isipokuwa huingia kwa yule Malaika, basi twaharisheni vinywa vyenu kwa ajili ya qur’ani) [ Imepokewa na Bazzar].
Faida za mswaki
Miongoni mwa faida za mswaki ni kuwa unasafisha kinywa duniani, na unamridhi Mwenyezi Mungu akhera. Nao unatia nguvu meno, unayashikanisha masinye, unatakasa sauti na unamchangamsha mja.
2.Kusukutua na kupuliza maji puani
Kusukutua
Kutia maji kinyawani na kuyatikisa.
Kupaliza puani
Kuyavuta maji puani kwa pumzi
Kusukutua
Kupaliza puani
3. Kutamba
Kutamba
Kuondoa athari ya kilichotoka kwenye tupu ya mbele au ya nyuma kwa maji yenye kutwahirisha. Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi: Ghuslu - MAANA YA KUSTANJI NA HUKMU YAKE
4. Kupunguza masharubu na kuyafanya madogo
Makusudio ni kuyapunguza sana, kwa kufanya hivyo kunapatikana uzuri na usafi na kuenda kinyume na makafiri.
5. Kufuga ndevu
Nako ni kuziacha na kutozigusa
Kunyoa ndevu
Ni haramu kunyoa ndevu, kwa amri iliyokuja ya kuzifuga na kuziacha.
Mtume ﷺ amesema: (Kateni masharubu na fugeni ndevu, wakhalifuni Majusi) [Imepokewa na Muslim.].
6.Kunyoa nywele sehemu za siri
Kunyoa nywele sehemu za siri (istihdad)
Kunyoa nywele zinazomea kandoni mwa tupu
Faida ya kunyoa nywele sehemu za siri
Imethubutu kielimu kwamba kunyoa
sehemu hizo kunatunza afya ya mwili, nguvu zake na usalama wake, kwa kuwa kule kuwa na nywele nyingi sehemu hii kunasababisha vijipu kwenye ngozi ambazo hudhuru mwili.
7. Kutahiri na kupasha tohara
Kumtahiri mwanamume
Ni kuondoa kigozi kinachofunika kichwa cha dhakari kwa mwanamume.
Kumpasha tohara mwanamke
Ni kukata kinyama kilichozidi kilichoko juu ya sehemu ya kuingiza dhakari ya mwanamume.
Kutahiri ni kwa mwanamume, na kupasha tohara ni kwa mwanamke kwa kuwa mtume ﷺ alimwambia Ummu Atiyyah: (Kata kidogo wala usifeke, kwani kufanya hivyo kunakufanya hapo mahali pawe na maangalizi mazuri na kunamfurahisha mume ) [ Imepokewa na Hakim].
Na kutahiri ni lazima kwa wanaume, ni sunna kwa wanawake.
Na hekima ya mwanamume kutahiriwa ni kuitwahirisha dhakari na najisi iliyopo kwenye kigozi kinachofunika kichwa cha dhakari. Ama kwa mwanamke ni kule kung’ara kwa uso wake
8. Kukata kucha
Nako ni kuzikata ili zisiwe ndefu
Kukata kucha
9. Kusumua nywele za makapwa
Yaani Kuondoa nywele zinazoota makapwani, kwa kuwa kuziondoa ni katika usafi na kuondoa harufu mbaya zinazokusanyika kwa kuwako nywele hizi.
Kusumua nywele za makapwa
10. Kuosha makunjo kwenye viungo
Makunjo viungoni
Viungo vya vidole
Baadhi ya wanavyuoni wameyaweka pamoja hayo makunjo na uchafu unaokusanyika masikioni na shingoni na baadhi ya sehemu za mwili.
Makunjo viungoni
Siku arubaini
Ni karaha kwa mtu kuacha kucha, pia nywele za makapwa, nywele sehemu za siri na masharubu zaidi ya siku arubaini. Imepokewa na Anas bin Malik t akisema: (Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alituwekea wakati wa kupunguza masharubu, kukata kucha, kunyoa nywele sehemu za siri na kusumua nywele za makapwa kuwa visiachwe zaidi ya siku arubaini) [Imepokewa na Muslim.].