Wudhuu Unatenguka Ukishika Damu Wakati Wa Kukata Nyama?

SWALI: asalam aleykum.kwanza kabisa namishukuruni kwa kutusaidia na kutujibu maswali yetu yanayo tupa matata.Mungu amijalie kila la kheri.swali langu mimi nikiwa na udhuu halafu nikikata kata nyama ina damu je udhuu wangu ninao?au mpaka nitawadhe tena?

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho Tumepokea Swali lako na jibu ni kwamba kukata nyama damu ikakakugusa sio jambo la kuvunja wudhuu. Ingia katika viungo vifuatavyo ambavyo vina maelezo kamili ya yale yanayovunja wudhuu.
Vitambulisho: