Surah Gani Kusoma Katika Swalah Ya Tahajjud Na Witr?

SWALI: Salaam Aleiqum, Ningependelea kujua ni sura gani hasa zilizosuniwa katika sala ya witri? Ukiwacha SABIH Ahsante

JIBU: بسم الله الرحمن الرحيم الحمد لله والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء والمرسلين وعلى آله وصحبه أجمعين و بعد Kuhusu Swalah ya Witr, ilikuwa ni Sunnah ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kuswali Raka'ah mbili mbili usiku na kumalizia kwa Raka'ah tatu za Witr na kufikia jumla ya Raka'ah zote kuwa kumi na moja kama ilivyokuja katika Hadiyth ifuatayo kutoka kwa Bibi 'Aishah: عن عائشة رضي الله عنها قال: ((ما كان يزيد في رمضان ولا غيره على إحدى عشرة ركعة، يصلي أربعًا، فلا تسأل عن حسنهن وطولهن، ثم يصلي أربعًا، فلا تسأل عن حسنهن وطولهن، ثم يصلي ثلاثًا)) البخاري و مسلم Kutoka kwa Bi 'Aishah ((Hajapata Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kuzidisha katika Ramadhaan wala miezi mingine zaidi ya Raka'ah kumi na moja, akiswali nne, wala usiulize uzuri wake na urefu wake, kisha akiswali nne wala usiulize uzuri wake na urefu wake, kisha akiswali tatu)) [Al-Bukhariy na Muslim] Na kuhusu Sura alizokuwa akisoma katika Swalatul-Witr zimethibiti katika Hadiyth hii ifuatayo: Hadiyth kutoka kwa Bibi 'Aishah رضي الله عنها ambaye amesema ((Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akisoma katika Raka'ah ya mwanzo ya (Swalah) Witr 'Sabbihisma Rabikal-A'ala' na Raka'ah ya pili 'Qul-Yaa-Ayyuhal-Kaafiruun' na Raka'ah ya tatu 'Qul- Huwa-Allaahu Ahad pamoja na Qul-A'udhu mbili (Al Falaq na An Naas)' [At Tirmidhiy] Na Allaah Anajua zaidi
Vitambulisho: