Mnyama wa kudhahi (kuchinja siku ya Idd)

9155

 

Maana ya mnyama wa Udh’hiya

Mnyama wa kudhahi

Ni yule anayechinjwa miongoni mwa wanyama howa siku za idd ya kuchinja kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.

Hukumu ya kudhahi

Ni sunna iliyotiliwa mkazo, kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Basi mswalie Mola wako na uchinje} [108: 20].

Na kwa hadithi ya Anas t kwamba Nabii (saw) alidhahi (alichinja) kondoo wawili wazuri [ Amlah: Mnyama mwenye weupe na weusi, na weupe ukawa ni mwingi zaidi.] wenye pembe [ Aqran: mwenye pembe.]. Aliwachinja kwa mkono wake. Akapiga bismillahi na akaleta takbiri na akaweka guu lake juu mbavu zao [Swifaahuhumaa: ni wingi wa swafhah nao ni upande wa shingo.]) [ Imepokewa na Tirmidhi].

Wakati wa kuchinja mnyama wa Udh’hiya

Wakati wa kuchinja unaanza baada ya Swala ya Idd ya kuchinga mpaka jua la siku ya mwisho wa siku za tashriiq kuzama (Siku ya kumi na moja, kumi nambili na kumi na tatu za mwezi wa Mfungotatu).

Mnyama wa Udh’hiya anayetosheleza

1. Mbuzi au kondoo mmoja anamtosheleza mtu mmoja. Na anaweza kumshirikisha anayemtaka katika thawabu, kwa kuwa Mtume alipotaka kuchinja mnyama wake wa kudhahi alisema: (Bismillahi. Ewe Mola mtakabalie Muhammad na jamaa za Muhammad na umma wa Muhammad) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2. Ngamia mmoja na ng’ombe mmoja wanawatosheleza watu saba. Basi yafaa kwa watu saba kushirikiana katika ngamia au ng’ombe, kwa kauli ya Jabir: (Akatuamrisha Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ tushirikiane katika ngamia na ng’ombe, kila watu saba miongoni mwetu kwa ngamia mmoja [Badanah: ni ngamia, awe ni mwanamke au mwanamke.] ) [Imepokewa na Muslim.].

Miaka ya mnyama inayotosheleza kwa Udh’hiya

Jadha› wa kondoo: Naye ni mwenye miezi sita.

Thanii wa mbuzi: ni mwenye mwaka mmoja.

Thanii wa ng’ombe: ni mwenye miaka miwili.

Thanii wa ngamia: ni mwenye miaka mitano.

Mnyama bora wa Udh’hiya

Mnyama bora ni ngamia ikiwa atatolewa mzima kwa sababu thamani yake iko juu na nimanufaa kwa mafakiri kisha ni Ngo;mbe ikiwa atatolewa mzima kisha Mbuzi, kisha fungu la saba la Ngamia kisha fungu la saba la Ngo’mbe

Aibu za mnyama wa Udh’hiya

1. Aibu zinazozuia kutosheleza [ Inazuilia kutosheleza: Haisihi kumchinja kama mnyama wa kudhahi.]

‹Awraa’: Ni mnyama mwenye ila machoni mwake, na anaingia ndani ya huyo mnyama kipofu.

‹Arjaa›: Ni mnyama asiyeweza kutembea.

‹Ajfaa’: Ni mnyama aliyekonda asiye na mafuta.

mgonjwa ambaye ugonjwa wake uko wazi:

Dalili ya hayo ni Hadithi iliyopokewa na Baraa› bin ‹Aazib t kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema: (Haifai kudhahi kwa mnyama mwenye jicho moja ambaye kasoro katika jicho lake iko wazi, na mnyama kiguru ambaye kiguru chake kiko wazi, na mngonjwa ambaye ugonjwa wake uko wazi, na aliyekonda asiye na mafuta [ Laa tanqii: hana duhu (mafuta).] ) [Imepokewa na Muslim.].

Na zinakutanishwa na hizi, aibu ambazo hufanana na hizi au ni mbaya zaidi kuliko hizi.

Aliyekonda
Kipofu wa jicho moja
Kiguru

2. Aibu zisizozuia kutosheleza kudhahi

AL-Batraa›: Asiye na mkia.

AL-Jammaa›: asiye na pembe kimaumbile.

AL-Khaswiyy: Kondoo ailiyekatwa konde zake za dhakari.

Alie na mpasuko kwenye sikio lake au tundu, au pembe yake imevunjika.

Haya yaliyotajwa kuhusu kinachotosheleza katika kudhahi ndiyo hayo hayo kuhusu tunuku na fidia.

Aliyevunjika pembe
Asiye na pembe
Asiekuwa na mkia

Kugawanya nyama ya Udh’hiya

Imeruhusiwa na sharia kwa mwenye kudhahi ale theluthi ya nyama yake, na akiitoa sadaka yote inafaa, na akila nyingi ya ile nyama pia inafaa.

Faida

Mwenye kutaka kudhahi, haifai akate nywele zake na kucha zake na kitu chochote mwilini mwake ungiapo mwezi wa Mfungotatu mapaka achinje. Hii ni kwa hadithi iliyopokewa na Ummu Salama t kwamba Mtume (saw) alisema: (Siku kumi zinapoingia na akataka mmoja wenu kudhahi, basi asiondowe chochote katika nywele zake na mwili wake) [Imepokewa na Muslim.].

Ama wale ambao wanafanyiwa tendo la kudhahi, kama mke na watoto, si haramu kwao kuondoa nywele au uchafu wa mwilini kama kucha.