makka na sehemu ya ibada ya hijja

7238

 

Tarehe ya Makka na hali ilivyokuwa na ilivyo sasa

Makka

Ni jina linalotokana na neno (bakka) lugha ya Kisamia ambalo maana yake ni bonde

Neno la Makka pia limekuja kwa tamshi la Bakka katika neno la Mwenyezi Mungu : {Hakika nyumba ya kwanza iliyowekewa watu ni iliyo Bakka, hali ya kuwa ni yenye baraka na uongofu kwa viumbe wote} [3: 96].

Tarehe ya Makka inakwenda nyuma hadi karne ya kumi na tisa kabla ya kuzaliwa Mtume Issa u, katika kipindi cha bwana wetu Ibrahim na Ismail, amani ziwashukie, kwani walikuwa ni watu wa mwanzo wa kukaa hapo. Mwenyezi Mungu U Anasema, Akimtolea hikaya Ibrahim: {Mola wetu! Hakika mimi nimewakilisha watu wa nyumbani kwangu kwenye ardhi isiyokuwa na mazao, kwenye Nyumba yako tukufu, ewe Molawetu!, ili watekeleze Swala. Basi zifanye nyoyo za watu ziwaelekee wao kwa mapenzi na uwaruzuku matunda ili washukuru} [14: 37].

Na kwa fadhila ya dua ya bwana wetu Ibrahim u yalitembuka maji ya Zamzamu kutoka chini ya nyayo za Ismail u alipomalizikiwa na maji na chakula mama yake, Hajara. Na kutoka wakati huo, makabila yalikusudia kuja hapo kwenye maji, na mahali hapo pakaanza uhai.

Na makabila yakaendelea kuja hapo na kuzaana, mpaka utawala wa mahali hapo ukaja kwa Makureshi. Na Makureshi wakaendelea kutawala mpaka kudhihiri Nabii Mohammed(saw) ambaye alikuwa na athari kubwa zaidi katika kugeuza maisha ya Makka tukufu na ulimwenguni kote.

Nabii Mohammed (saw) alitumilizwa Makka, na Alkaba ikawa ni kibla cha Waislamu, na Makka ikawa ndio kituo cha ulinganizi wa Kiislamu, lakini watu wake walikuwa wakali zaidi katika kuwaepusha watu na Uislamu na kuwaadhibu waliosilimu, mpaka wakalazimika Waislamu kuhamia Madina iliyonawirishwa, na dola ya Kiislamu ikasimama huko. Kisha Mtume (saw) akarudi Makka kuikomboa, ikawa kuanzia wakati huo, ni mji mkubwa wa Kiislamu mpaka zama zetu hizi.

Na kwahakika mji wa Makka ulipata umuhimu mkubwa kutoka kwa makhalifa na viongozi wakiislamu. Na wakajitolea kujenga Makka na kuupanua mji, na wakafanya makka ni kituo cha kusambaza nuru ya Dina ya Kiisalamu katika ulimwengu wote

Utukufu wa Makkah

1. Ni amani kwa anayeingia

Mwenyezi Mungu U Anasema: {Na Mwenye kuingia atakuwa kwenye amani} [3: 97], yaani Haramu ya Makka.

2. Haingi Dajjaal mji wa Makka, wala magonjwa hatari yenye kuambukiza na kuua.

Abu Huraira t amepokewa akisema kwamba Mtume (saw) alisema: (Madina na Makka imezungukwa na Malika, katika kila pembe [ Naqab: njia.] yake kuna Malaika. Haingiliwi na Dajjaal wala magonjwa hatari ya kuambukiza na kuua) [Imepokewa na Ahmad.].

3. Kuswali kwenye Msikiti wa Haram thawabu zake ni Swala elfu mia moja.

Jabir t alipokewa akisema kuwa Mtume (saw) alisema: (Swala moja ndani ya Msikiti wa Haramu ni bora kuliko Swala elfu mia moja katika misikiti mingine) [Imepokewa na Ibnu Maajah.].

4. Makka ni ardhi inayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu U

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu(saw): (Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Wewe ni ardhi ya Mwenyezi Mungu njema zaidi, na ni ardhi ya Mwenyezi Mungu inayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu) [Imepokewa na Tirmidhi.].

Hukumu zinazohusu Makka peke yake na eneo la Haram

1. Onyo kali kwa anayetia nia kufanya ovu huko Haram, awe amelifanya au hakulifanya

Mwenyezi Mungu U Amesema: {Na yoyote mwenye kutaka kupotoka na kuleta udhalimu huko, basi tutamuonjesha adhabu kali} [22: 25].

Imepokewa na Ibn Abbas t kuotoka kwa Mtume (saw) Akisema: (Watu wanaochukiwa sana na Mwenyezi Mungu ni watu watatu) na akataja miongoni mwao ni (Mwenye kupotoka -kupinga Sharia ya Mwenyezi Mungu- katika Haram) [Imepokewa na Bukhari.].

Makka

2. Uharamu wa kupigana na kumwaga damu humo

Amesema Mwenyezi Mungu (saw): {Na tulipoijaalia Nyumba ni mahali pa watu kukusanyika na mahali pa amani} [2: 125].

Mwenye kuingia Makka ataaminika humo, kwa neno la Mtume (saw): (Si halali kwa mmoja wenu kubeba silaha Makka) [Imepokewa na Muslim.].

Na amesema Mtume (saw): (Mwenyezi Mungu Ameiharamisha Makka na si watu walioiharamisha. Kwa hivyo, si halali kwa anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kumwaga damu huko wala kukata mti) [Imepokewa na Bukhari.]

Kuuwa na kumwaga damu

3. Kuharamishwa kuingia makafiri na mushrikina haram ya Makka

Amesema Mwenyezi Mungu U: {Enyi mlioamini! Hakika washirikina ni najisi, basi wasikaribie Msikiti wa Haram (Makka) baada ya mwaka wao huu} [9: 28].

Na Mtume (saw) aliamrisha nayeye yuko Mina kutangazwe: (Asihiji mshirikina baada ya mwaka huu, na asitufu Al-Ka’ba mtu akiwa uchi) [Imepokewa na Bukhari.].

4. Uharamishaji wa kuwinda, kukata miti na kuokota kwenye Haram ila kwa mwenye kukijulisha

Ibnu ‹Abbas t alipokewa kutoka kwa Mtume (saw) akisema: (Mwenyezi Mungu Ameiharamisha Makka, si halali kwa yoyote kabla yangu wala kwa yoyote baada yangu. Mimi nilihalalishiwa kipindi kichache cha mchana. Mimea yake mibichi haikatwi, na pia miti yake haikatwi, na kiwindwa chake hakifukuzwi, na kilichopotea chake hakiokotwi isipokuwa kwa mwenye kukitangaza) [Imepokewa na Bukhari.].

Sehemu za ibada ya hija

1. Arafaat

Arafaat: ni wingi wa Arafah. Na imeitwa hivyo kwa kuwa Adam na Hawa walijuana hapo, au kwa kuwa watu hapo hukiri makosa yao.

Napo ni mojawapo ya alama iliyo nje ya mipaka ya Haram. Na iko upande wa Kusini Mashariki wa Msikiti wa Haram kwa umbali wa kilomita ishirini. Na jumla ya eneo lake ni kilomita 10, 4 mraba, n hapo mahujaji wanakusanyika siku ya tisa ya Mfungotatu.

Arafaat

Msikiti wa Namirah

Namirah: ni jabali lilioko upande wa Magharibi wa Msikiti, na kwa sababu ya jabali hilo msikiti unaitwa msikiti wa Namirah.

Na Mtume (saw) alishuka hapo kwenye bonde la ‘Urana, akahutubu na akaswali, na ukajengwa msikiti pale alipohutubu na kuswali, katikati ya bonde la ‘Urana mwanzo wa ukhalifa wa Kiabasia. Na ulimalizika kupanuliwa na kuuamirisha katika kipindi cha ufalme wa Kisuudi, mpaka likafikia eneo lake zaidi ya mita 110 mraba. Na mahujaji wanakusanyika hapo terehe tisa ya Mfungotatu.

Masjid Namirah

Msikiti wa Swakharaat

Nao uko Arafa, chini ya Jabali la Rehema upande wa kulia wa mwenye kulipanda. Na hapo pana mawe makubwa ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisimama hapo jioni ya siku ya Arafa. Mahujaji wanakusanyika hapo siku ya tisa ya Mfungotatu..

Masjid Swakharaat

Jabali la Rehema

Ni jabali dogo lenye jiwe kubwa, liko umbali wa kilo ishirini Mashariki ya Makka, na ardhi yake imelingana sawa pana. Na mzunguko wake ni kilomita 640 mraba. Mahujaji wanakusanyika hapo siku ya tisa ya Mfungotatu.

Jabalu-Rahma

2. Mina

Iliitwa Mina kwa sababu ya damu zinazomwagwa.

Nayo iko baina ya Makka na Muzdalifa kwa umbali wa kilomita saba, Mashariki ya Msikiti wa Haram. Mahujaji wanalala hapo masiku ya tarehe 11-12 ya Mfungotatu kwa anayefanya haraka, na usiku wa 13 kwa anayejichelewesha. Napo ni mahali pa ibada ya Hija palioko ndani ya mipaka ya Haram. Na hapo pana Msikiti wa Khiif, na jamaraat, sehemu ya kutupa vijiwe

Mina

Jamaraat

Na viguzo vitatu vya ibada ya Hija hapo Mina ni: Kiguzo kidogo, cha katinakati na cha mwisho, nazo ni viguzo vya mawe vilivyo ndani ya mabirika matatu, vikiwa ni alama ya mahali alipodhihiri Shetani na bwana wetu Ibrahim akamrushia mawe. Na masafa baina ya kiguzo cha mwisho na cha kati ni kadiri ya mita 247, na baina ya cha katinakati na kidogo ni kadiri ya mita 200.

Msikiti wa Khaif

Uko kwenye kilele cha jabali la Mina lilioko upande wa kusini, karibu ya Kiguzo kidogo.

Msikiti wa Khiif

3. Muzdalifa

Muzdalifa ni mahali baina ya Mina na Arafa. Hapo Mahujaji wanalala baada kusimama Arafa.

Na katikati ya Muzdalifa kuna al-Mash’ar al-Haraam, napo mahali panapopendekezwa Mahujaji wasimame hapo wamuombe Mola wao Aliyetukuka, wamtaje na wamshukuru. Na hapo ni malazi ya mahujaji wanapoteremka kutoka Arafa baada ya jua kuzama la tarehe 9 ya mfungotatu.

Muzdalifa

4.Msikiti wa Haraam

Alkaba tukufu

Alkaba tukufu vile ilivyo ni kichemraba

Hijri ya Ismail

Nayo ni sehemu ya upande wa kaskazini wa Alkaba ambao matumizi ya Makureshi yalishindwa kumaliza ujenzi walipotaka kuijenga Alkaba, wakaweka ukuta uliyozunguka upande mmoja ili kutanabahisha kuwa sehemu hiyo ni ya Alkaba. Na jina hili ni la kupewa na watu si la kisheria.

Jiwe Leusi

Nalo liko kwenye nguzo ya upande wa kusini wa Alkaba tukufu, nalo linatoka Peponi. Na Jiwe Leusi limevunjikavunjika halikusalia isipokuwa vijiwe vinane vidogo sana kama mbae za tende.

Nguzo ya upande wa Yaman

Nayo ni nguzo ya Alkaba iliyoko upande wa kusini Magharibi, na inaitwa Nguzo ya Yamani, kwa kuwa iko kwenye mkabala wa yamani. Na miongoni mwa mambo yanayohusika na nguzo ya yamani ni kuwa iko kwenye misingi ya mwanzo ya Alkaba iliyoinuliwa na Ibrahim na ismail, amani iwashukie.

Multazam

Nayo ni sehemu iliyo baina ya Jiwe Leusi na mlango wa Alkaba. Na kadiri yake ni mita mbili. Napo ni mahali pa kuitikiwa dua. Imesuniwa kuomba dua hapo pamoja na kuambatisha mashavu, kifua, mikono na vitanga vya mikono.

Jiwe Leusi
Nguzo ya upande wa Yamani
Multazam