Nguzo, Wajibu na Sunna za Hija

13559

 

Nguzo za Hijja

1. Kuhirimia:

kwa neno la Mtume (saw): ( Hakika matendo mema yategemea nia, na hakika kila mtu atapata lile alilonuilia) [Imepokewa na Bukhari.].

2. Kusai baina ya Swafaa na Marwah:

kwa neno lake (saw): (Saini, kwani Mwenyezi Mungu Amewafaradhia kusai) [Imepokewa na Ahmad.].

3. Kusimama Arafa:

kwa kauli ya Mtume (saw): (Hija ni Arafa) [Imepokewa na Tirmidhi.].

4. Twawafu ya Ifaadhah:

kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Na ili waitufu Nyumba ya Zamani} [22: 29].

- Tanabahisho

Mwenye kuacha nguzo moja miongoni mwa nguzo za Hijja, ikiwa ni kuhirimia basi ibada yake haikubaliki kwa sababu hakutia nia na ibada haikubaliki bila ya nia na ikwa ni nguzo nyingine ya Hijja haitatimia mpaka ailete.

Wajibu za Hijja

1. Kuhirimia kwenye sehemu zilizowekwa kuhirimia:

kwa neno lake (saw) baada ya kuzitaja sehemu za kuhirimia: (Hizo ni za watu wa sehemu hizo na wale wanaokuja hapo kati ya watu wa sehemu nyingine miongoni mwa wale wanataka kuhiji au kufanya Umra) [Imepokewa na Bukhari].

2. Kusimama Arafa mpaka jua kuzama kwa aliyesimama mchana:

Kwa kuwa Nabii (saw) alisimama mpaka jua likazama.

3. Kulala hapo Muzdalifa:

kwa sababu Mtume (saw) alilala hapo na akasema: (Umma wangu wachukue ibada yao ya Hija kutoka kwangu, kwani mimi sijui pengine huenda nisikutane nao baada ya mwaka wangu huu) [Imepokewa na Ibnu Maja.].

Na kwamba yeye (saw) aliwaruhusu Waislamu madhaifu baada ya nusu ya usiku. Hilo linaonyesha kwamba kulala hapo Muzdalifa ni lazima. Na Mwenyezi Mungu Ameamrisha atajwe katika Mash’ar al-Haraam.

4. Kulala Mina masiku ya siku za tashriiq:

kwa ilivyothubutu kwamba Nabii (saw) aliwaruhusu wachungaji kulala kando ya Mina [Imepokewa na Abu Ya›laa katika Musnad yake.].

Hii inaonyesha kwamba asili ni kuwa kulala Mina ni wajibu.

5. Kuvirushia viguzo vijiwe,

kwa kauli Yake Aliyetukuka: {Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika siku zinazohesabika} [2: 203].

Na siku zinazohesabika: ni siku za ashriiq.

Na kurusha vijiwe ni miongoni mwa kumtaja Mwenyezi Mungu, kwa neno la Mtume (saw): (Hakika kutufu Alkaba, kusai baina ya Swafaa na Marwah na kuvirushia viguzo vijiwe ni miongoni mwa kusimamisha utajo wa Mwenyezi Mungu) [Imepokewa na Abu Daud.].

6. Kunyoa au kupunguza,

kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Mtaingia- mtaingia Msikiti wa Haram mkiwa kwenye amani, Mwenyezi Mungu Atakapo, hali ya kunyoa vichwa vyenu na kupunguza} [48: 27].

7. Kutufu twawafu ya kuaga:

kwa haditi iliyothubutu kutoka kwa Ibnu ‘Abbas t kuwa alisema: (Wameamrishwa watu kuwe kule kutufu twawafu ya kuaga iwe shughuli yao ya mwisho kwenye Alkaba, isipokuwa mwenye hedhi alirahisishiwa) [Imepokewa na Muslim].

Sunna za Hijja

Lisilokuwa nguzo na wajibu ni Sunna, kama inavyofuata:

1. Kuoga wakati wa kuhirimia.

2. Kuhirimia kwa kikoi cheupe na shuka ya juu nyeupe.

3. Kuleta Labeka kwa sauti ya juu.

4. Kutufu twawafu ya kufika Makka kwa anayechanganya Hija na Umra na anayehiji peke yake.

5. Kwenda haraka katika mizunguko mitatu ya mwanzo twawafu ya kufika Makka (kwa ibada ya Hija) au Umra. Ramal ni kutembea kwa haraka.

6. Kufanya idhtibaa’ katika twawafu ya kufika Makka (kwa mwenye kuhiji) au Umra, nako ni kuiweka shuka yake ya juu chini ya kapwa la mkono wa kulia.

7. Kulala Mina usiku wa Arafa.

8. Kulibusu Jiwe Leusi.

9. Kukusanya swala ya Maghrib na isha katika Muzdalifa kwa kuchelewesh

10. Kusimama Muzdalifa kwenye mash’aril haraam kuanzia Alfajiri mpa karibu na kuchomoza jua akiweza kufanaya hivyo, asipo weza sehemu yoyote ya Muzdalifa ni sehemu yakisimamo.

Sunna za Hijja

Mwenye kuiacha sunna moja miongoni mwa sunna za Hija, halazimiwi na kitu chochote, na Hija yake ni sahihi.

Wajibu wa Hajji

Mwenye kuacha wajibu itamlazimu kuchinja mnyama ili kuunga upungufu huu.