tok99toto slot zeus slot thailand slot gacor ladangtoto ladangtoto link alternatif ok88 deposit dana https://ladangtoto.bintangara.tabalongkab.go.id/ klik88 cara login ladangtoto terbaru ladangtoto rtp maxwin https://ladangtoto.nbagroup.co.id/ https://dewaslot.nbagroup.co.id/ link alternatif indoslot ladangtoto terbaru klik88 rtp maxwin https://slot-thailand.telusur.co.id/ slot thailand 66kbet slot gacor mahjong slot gacor mahjong ladangtoto ying77 maxwin link ladangtoto login link masuk 66kbet link masuk klik88 link masuk ying77 slot gacor server thailand link situs ladangtoto gacor88 link 66kbet gacor88 server thailand super gacor login ladangtoto situs togel ladangtoto link alternatif ladangtoto situs ladangtoto2 66kbet game terpopuler ying77 game terpopuler mahjong ways terbaru ying77 server thailand 66kbet deposit 5k slot thailand sbobet 2023 slot joker123 2023 slot mahjong ways 2023 ladangtoto terbaru dan terpopuler sv388 sabung ayam digmaan 2023 ok88 terbaik ladangtoto togel 2023 joker123 login slot 777 gacor maxwin pg soft login ladangtoto slot gacor link alternatif ok88slot link ok88slot mahjong ways ladangtoto login alternatif 66kbet login alternatif ying77 login alternatif 888slot login alternatif gb777 login alternatif gacor88 rtp gacor slot server kamboja nolimit city slot deposit bsi slot mahjong pg slot slot depo 10k slot depo 10k slot gopay server thailand super gacor slot ovo slot kakek zeus slot deposit pulsa slot dana slot neobank slot depo 5k slot jepang slot cq0 slot maxwin https://starlight-princess.rumahsakitakgani.co.id/ http://sweet-bonanza.rumahsakitakgani.co.id/ ladangtoto official gacor88 official site Situs Resmi Products Gacor88 ladangtoto maxwin link login slot ladangtoto link togel ladangtoto ladangtoto server thailand ladangtoto togel bet 100 daftar togel ladangtoto togel ladangtoto terbaik rtp area178 https://joker123.abhatigroup.com/ https://pg-slot.abhatigroup.com/ RajaJp Official https://raja88.abhatigroup.com/ https://ladangtoto.alfabeauty.co.id/ https://66kbet.abhatigroup.com/ https://habanero.alfabeauty.co.id/ https://spadegaming.alfabeauty.co.id/ ying77 terbaik tok99toto link https://66kbet.alfabeauty.co.id/ https://ladangtoto.grandsukatani.co.id/ klikslot88 one8slot gacor klikslot88 maxwin https://pg-soft.telusur.co.id/ ladangtoto terpercaya https://ladangtoto.pt-kcb.co.id/ https://ok88.sasakala.id https://kinokuniya.co.id/modules/ladangtoto/ https://ladangtoto.sasakala.id/ https://ok88.rumahsakitakgani.co.id/ https://gacor88.pt-kcb.co.id/ https://ladangtoto.pt-kcb.co.id/ https://raja88jp.abhatiland.com/ klik88slot super gacor link slot gacor ok88 ladangtoto login https://slot-dana.ppak.co.id/ 888slot maxwin slot777 situs slot gacor server thailand https://data-hk.ppak.co.id/ ladangtoto2 daftar joker gaming link slot88 https://ladangtoto.banknusumma.co.id/ Link Joker123 https://stietribuana.ac.id/wp-includes/js/products/ladangtoto/ https://stietribuana.ac.id/wp-includes/js/products/slot thailand/ https://slot88.nasuha.uinjambi.ac.id/ https://ladangtoto.stikesbantul.ac.id/ https://indonesia.nasuha.uinjambi.ac.id/ https://indonesia.nasuha.uinjambi.ac.id/toto/ https://indonesia.nasuha.uinjambi.ac.id/idn/ https://indonesia.nasuha.uinjambi.ac.id/data-macau/ https://sbobet.nasuha.uinjambi.ac.id/ https://ladangtoto.nasuha.uinjambi.ac.id/ https://bkd.keeromkab.go.id/ https://ladangtoto.eracakrawalaindonesia.co.id/ https://ladangtoto.wisatamedis.id/ https://slot77.ppak.co.id/ https://pdd.angkolasangkunur.tapselkab.go.id/ https://pdd.angkolasangkunur.tapselkab.go.id/depo10k/ https://pdd.angkolasangkunur.tapselkab.go.id/depo5k/ https://css.angkolasangkunur.tapselkab.go.id/ https://visi.angkolasangkunur.tapselkab.go.id/ https://aptr.angkolasangkunur.tapselkab.go.id/ https://jbpe.angkolasangkunur.tapselkab.go.id/ https://slot-olympus.uptkukm.id/ https://slot-mahjong.uptkukm.id/ https://slot-zeus.uptkukm.id/ https://slot-thailand.uptkukm.id/ https://data-macau.uptkukm.id/ https://slot-joker.uptkukm.id/ https://data-sdy.uptkukm.id/ https://data-hk.uptkukm.id/ https://pgpaud.fkip.untad.ac.id/phei/server-thailand/ https://server-thailand.pa-paniai.go.id/ https://gopay.pa-paniai.go.id/ https://maxwin.pa-paniai.go.id/ https://depo5k.pa-paniai.go.id/ https://depo10k.pa-paniai.go.id/ https://ladangtoto.pa-paniai.go.id/ https://joker123.pa-paniai.go.id/ https://depo-ovo.pa-paniai.go.id/ https://spaceman.pa-paniai.go.id/ https://lucky-neko.pa-paniai.go.id/ https://66kbet.rumahjurnal.or.id/ https://888slot.rumahjurnal.or.id/ https://data-hk.rumahjurnal.or.id/ https://data-sdy.rumahjurnal.or.id/ https://data-macau.rumahjurnal.or.id/ https://slot-idn.rumahjurnal.or.id/ https://gopay.stikesbantul.ac.id/ https://sv388.stikesbantul.ac.id/ slot deposit dana slot zeus slot bca slot777 super gacor maxwin malam ini https://portal.kejari-cirebonkab.go.id/ https://perpustakaan.umk.ac.id/shop/zeus-maxwin/ https://perpustakaan.umk.ac.id/shop/server-thailand/ https://ladangtoto.triomotor.co.id/ https://gb777.gkindonesia.id/ https://k86sport.gkindonesia.id/ https://klik88slot.gkindonesia.id/ https://ying77.gkindonesia.id/ https://888slot.gkindonesia.id/ https://66kbet.gkindonesia.id/ https://tok99toto.gkindonesia.id/ https://ladangtoto.gkindonesia.id/ https://icon-eltl.unila.ac.id/slot77/ https://icon-eltl.unila.ac.id/server-thailand/ klik88 situs slot thailand Istihaadhwah (Damu Inayoendelea baada ya Hedhi) Na Hukumu Zake- utwahara


Istihaadhwah (Damu Inayoendelea baada ya Hedhi) Na Hukumu Zake

SWALI LA KWANZA: asalamu aleykum NAOMBA MUNISAIDIYE TATIZO LANGU NAPATA HEDHI KWA KUDA MREFU SIKU 24 HADI MWENZI SASA NATAKA KUJUA BAADA YA SIKU NGAPI NAWEZA KUFUNGA NA KUSWALI MANA NIMESIKIA BAADA YA MDA KADHAA HUWA NI MARADHI KWAHIYO WAWEZA KUFUNGA NA KUSWALI inatoka kidogo kidogo inakuwa kama makruu NAOMBA MUNISAIDYE TATIZO HILO AHASANTUM WABILAH TAUFQ SWALI LA PILI: sheikh, mimi nauliza kama wapata hedhi mara mbili kwa mwezi hio huwa ni isthadhwa au nikitu kingine??

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Hali yako hiyo bila ya shaka itakuwa ni hali ya Istihaadhwah nayo ni damu inayomtoka mwanamke isiyokuwa ya hedhi au nifaas bali ni damu ya kawaida kwani haiwezekani mwanamke kuwa na hedhi siku zote hizo au hadi ifikie mwezi. Kwani ingawa Maulamaa wameona kuwa hakuna idadi maalumu za hedhi na nifaas na rai mbali mbali zimetolewa kuhusu muda au damu ya hedhi na nifaas kama ifuatavyo: 1. Mwanamke ahesabu idadi ya siku zake za hedhi za kawaida yake ilivyo mfano kama ni siku saba basi akifikisha ya nane afanye ghuslu zilizobakia ni Istihaadhwah. 2. Ikiwa ni kawaida yake ya hedhi siku saba basi asubiri hadi apitishe siku kumi na tano. 3. Atazame sifa za damu zifuatazo ili aweze kutofautisha baina ya damu ya hedhi na ya Istihaadhwah: Rangi: Damu ya hedhi huwa ni nyekundu iliyoiva kukaribia kuwa nyeusi na damu ya Istihaadhwah ni nyekundu inayong'aa (bright red) Shakili yake: Damu ya hedhi huwa nzito, ama ya Istihaadhwah huwa ni nyepesi. Harufu: Damu ya hedhi huwa ina harufu ya kukirihisha, ama damu ya Istihaadhwah haina harufu kwani huwa inatoka katika mishipa ya kawaida katika mwili wa binaadamu. Lakini kutokana na hali yako kufikisha siku ishirini na tano au mwezi basi hakuna shaka kuwa hiyo ni Istihaadhwah kwani sio twabi'iy (natural) mwanamke kuwa katika hedhi mwezi mzima takriban. Hivyo uhesabu ima idadi ya siku zako za kawaida kisha utazame kama damu inayotoka baada ya hapo inazo sifa zilizotajwa hapo juu au la. Au uhesabu siku kumi na tano kisha zilizobakia zitakuwa ni Istihaadhwah na utafuata hukmu za Istihaadhwah kama ifutavyo: Hukmu Za Istihaadhwah: Hukmu za Istihaadhwah ni sawa sawa na hukmu za mwanamke anapokuwa katika twahaarah yaani mwanamke asiyekuwa katika hedhi. Hivyo anatakiwa aswali na kufunga kama kawaida kama ilivyokuja dailili ifuatayo: عن عائشة قالت : جاءت فاطمة بنت أبي حبيش إلى النبي صلى الله عليه وسلم فقالت : يا رسول الله إني امرأة أستحاض فلا أطهر أفأدع الصلاة ؟ فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ ، إِنَّمَا ذَلك عِرْقٌ وَلَيْسَ بِحَيْضٍ ،فَإذا أَقْبَلتْ حَيْضتُكِ فَدَعِي الصَّلاةَ , وَإِذَا أَدْبَرتْ فَاغْسِلي عنكِ الدمَ ثُمَّ صَلِّي)) رواه البخاري ) ومسلم. Kutoka kwa Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba Faatwimah bint Hubaysh alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Ewe Mjumbe wa Allaah, mimi ni mwanamke ninayepatwa na Istihaadhwah, siwi katika twaaharah, je niache kuswali?" Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hapana huo ni mshipa tu na sio hedhi. Unapopata hedhi acha kuswali na inapomalizika osha damu [baada ya kufanya ghuslu) kisha Swali)) [Al-Bukhaariy na Muslim] Shaykh Ibn 'Uthaymiyn katika kuelezea maana yake kasema: "Ni mshipa tu. Hivyo inafahamika kwamba ikiwa damu inayotoka katika mshipa pamoja na damu inayomtoka mtu kutokana na operesehi haitambuliki kuwa ni damu ya hedhi. Kwa hiyo yanayokuwa haraam katika hedhi hayawezi kuwa haraam katika hali hii, na mwanamke anatakiwa aswali, afunge inapomfikia……Ramadhaan" [Majmuu' al-Fataawa Ibn 'Uthaymiyn 11/Swali Namba 226] وعن عائشة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم اعتكف معه بعض نسائه , وهي مستحاضة ترى الدم , فربما وضعت الطست تحتها من الدم . رواه البخاري. Na kutoka kwa Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikaa I'tikaaf na mke wake mmoja naye alikuwa katika Istihaadhwah akiona damu. Mara nyingine aliweka chombo kukingia damu)) [Al-Bukhaariy] Kutokana na hiyo Hadiyth pamoja na nyinginezo, ni dalili kwamba hakuna tofauti ya mwanamke mwenye Istihaadhwah na mwanamke asiyekuwa na hedhi isipokuwa yafuatayo: Wudhuu Kwa kila Swalah: Afanye wudhuu kwa kila Swalah kwa sababu Mtume alimwambia mkewe: ((…. Basi fanya wudhuu kwa kila Swalah)) [Al-Bukhaariy] Ina maana kwamba asifanye wudhuu mapema kabla ya Swalah kuwadia bali afanye wudhuu pale pale anapotaka kuswali. Kujisafisha kabla ya kufanya wudhuu: Anapotaka kufanya wudhuu kwanza ajisafishe vizuri na alama zote za damu ziondoke. Kisha ajiwekee pamba sehemu zake siri ili kuzuia damu isitoke wakati anaposwali kama Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyomwambia Hamnah: ( أنعت لك الكرسف , فإنه يذهب الدم)) ، قالت : فإنه أكثر من ذلك ، قال : ((فاتخذي ثوباً)) . قالت : هو أكثر من ذلك . قال ((فتلجمي)) الحديث ((Nakudokeza uweke kipande cha pamba kwani itanyonya damu)) Akasema (Hamnah): Ni zaidi ya hivyo [yaani haifai kitu damu bado inatoka]. Akasema (Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Tumia kitambaa)) Akasema: Ni zaidi ya hivyo: Akasema ((Basi ikaze vizuri nayo)) Akifanya hivyo mwanamke mwenye Istihaadhwah kisha ikitoka damu basi haitodhuru kitu kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Faatwimah bint Abi Hubaysh: ((اجتنبي الصلاة أيام حيضك ثم اغتسلي وتوضئي لكل صلاة ، ثم صلي ، وإن قطر الدم على الحصير)) رواه أحمد وابن ماجة . ((Acha kuswali wakati wa siku zako za hedhi, kisha fanya ghuslu na ufanye wudhuu kwa kila Swalah hata damu ikimwagika katika mswala)) [Ahmad na Ibn Maajah] Maingiliano na mume: Maulamaa wamekhitilafiana kuhusu kuruhusiwa jimai (kitendo cha ndoa) ikiwa hakutakuwa na mashaka ya kuacha kabisa. Lakini rai iliyo Swahiyh ni kwamba inaruhusiwa katika kila hali kwa sababu kwanza wanawake wengi walikuwa wakipata Istihaadhwah zama za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na wala hakukuwa na makatazo kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) au Mjumbe Wake kuwakataza jimai bali kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala): ((فَاعْتَزِلُواْ النِّسَاء فِي الْمَحِيضِ)) ((Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi)) [Al-Baqarah: 222] inafahamika kwamba haikukatazwa kujitenga nao nyakati nyinginezo. Na ikiwa wameruhusiwa kuswali basi kufanya jimai ni tendo lisilo na uzito sana kama kuacha kuswali. Haitokuwa sawa kama italinganishwa kwa kupima kwa Qiyaas (analogy) baina ya kujimai na mwanamke aliyekuwa katika Istihaadhwah kuwa ni sawa sawa kwa sababu uhakika ni kwamba hawako sawa japo kuwa wengine rai zao wameona kuwa ni haraam. ['Risaalah fid-dimaa' at-twaabi'iyyah lin-Nisaa' - Shaykh Ibn 'Uthaymiyn - “Risala Kuhusu Damu Za Maumbile Za Wanawake” ya Shaykh Ibn ‘Uthaymiyn] Na makala hii ndefu ya “Risala Kuhusu Damu Za Maumbile Za Wanawake” ya Shaykh Ibn ‘Uthaymiyn imetafsiriwa kwa lugha ya kiswahili ambayo imewekwa katika kitabu kidogo ambacho kinapatikana katika maduka ya vitabu vya Dini mjini Dar-es-Salaam. Ni kitabu kizuri ambacho kinamama wanapaswa kuwa nacho inshaAllaah Soma pia Maswali Na Majibu katika viungo vifuatavyo upate maelezo na faida zaidi: Nimepata Hedhi Karibu Magharibi Je Nilipe Swawm? Damu Inayotoka Akiwa Mja Mzito Ni Kama Ya Hedhi Je Aswali? Na Allaah Anajua zaidi




Vitambulisho: