Imaam Al-Albaaniy - Hajjaaj Bin Yuwsuf Alikuwa Kafiri?

SWALI: Nini lililo sahihi kuhusu Al-Hajjaaj bin Yuwsuf Ath-Thaqafiy? Je, alikuwa kafiri?

JIBU: Tunashuhudia kwamba Al-Hajjaaj alikuwa 'asi mtenda dhambi na dhalimu. Lakini hatujui kama alikanusha lolote katika Dini ambayo ni mambo ya dharura yanayojulikana katika Dini. Kwa hiyo, haijuzu kumkufurisha kwa sababu tu ya kuwa yeye alikuwa ni asi na dhalimu na kuua waja wema katika Waislamu. [Fataawa Imaam Al-Albaaniy, Majallah Asw-Swaalah (10)]
Vitambulisho: