JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Inapokuwa hali kama hiyo ya kutokwa na manii japo kidogo hata bila ya tupu kugusana, basi itakubidi ukoge josho (ghuslu) kwani kutokwa na manii kwa shahwa ikiwa umelala au umacho kwa mwanamke au mwanamume ni mojawapo ya mambo yanayompasa Muislam kuoga. Dalili ni hadiythi zifuatazo: Kutoka kwa Abu Sa'idy رضي الله عنه ambaye amesema kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: ((الماء من الماء)) مسلم ((Maji ni baada ya kutokwa na Maji)) (Maana kwamba maji ya mwanzo hapa ni kukoga, na Maji ya pili ni manii) [Muslim] Vile vile Hadiyth iliyoripotiwa na Ummu Salamah (Mama wa Waumini) kwamba Ummu Sulaym alisema: يا رسول الله، إن الله لا يستحي من الحق، فهل على المرأة غسل إذا احتلمت؟ قال :((نعم، إذا رأت الماء )) البخار و مسلم Ee Mjumbe wa Allaah, hakika Allaah Haoni haya na (mambo ya) haki. Je, Mwanamke anahitajika kukoga (ghuslu) akiota amejimwagia? Akasema: ((Ndio, atakapoona maji (manii))) [Al-Bukhaariy, Muslim].
Na Allaah Anajua zaidi
Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Ghuslu - Vipi Kukoga Janabah, Nifaas Na Hedhi