Kila kinachotoka ndani ya ardhi, na kinawezekana kunufaika nacho.
Kila kinachotoka ndani ya ardhi, na kinawezekana kunufaika nacho.
Kinachotoka ndani Ardhini ni Sampuli mbili: ni Nafaka na Matunda na Madini, na Hazina iliyozikwa Ardhini
Kila tembe (mbegu) inayohifadhiwa katika mtama, ngano na mfano wa hii.
Kila tunda linalohifadhiwa kama tende, na zabibu, na lozi.
Zaka ya nafaka na matunda ni wajibu, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: {Na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake} (Al-An-am: 141);
na kwa kauli ya Mtume (saw): (Kwa yaliyo nyunyiziwa (maji) ya mbinguni (yaani mvua) au mito au kama yamemea yenyewe [ Yamemea yenyewe: Ni mavuno yaliyomea kwa kunywa maji bila ya kunyunyuziwa maji, ima ni kwa unywevu wa mizizi yake kuwa na umajimaji au kupitia kwa mvua na umajimaji (kama vile hali ya umande) na mito.] (inafaa mtu atoe) ushuri moja (yaani atoe sehemu moja kwa kumi ya mavuno atakayopata (1/10), na yaliyonyunyiziwa kwa kumwagiwa maji [ Yaliyonyunyiziwa kwa kumwagiwa maji (na mtu mwenyewe): Yaani amemwagia maji na akagharamika katika kuyatoa hayo mavuno.] nusu ushuri (yaani atoe sehemu moja kwa tano yamavuno atakayopata (1/20)” [ Imepokewa na Bukhari.].
Ikiwa si mavuno ya kuhifadhika, na ni mavuno ya chakula chake cha siku basi hakuna Zaka ya kutolewa hapo; kwasababu sio ya kuhifadhiwa hayakuzidi mahitaji yake ya kula kwake kwa kila siku, hivyo basi hayamtoshelezi mahitaji yake; kwa kukosekana utulivu wa kunufaika (na yale mavuno).
Na hii iwe ni katika (mavuno) yanayopimwa kwa mizani ili kulinganishwa na saaq, nayo ni kipimo (fulani), hii inaashiria kutambulika kwa mavuno hayo; kwa kauli ya Mtume (saw): (Hakuna katika nafaka, wala tende Zaka yoyote mpaka ifike saaq tano [Al - Wasaq: Ni Sawa na Pishi 60.] ) [Imepokewa na Muslim.].
Basi ikiwa sio mavuno yanayopimwa kama vile mboga, na mabogaboga, hakuna Zaka kwa vitu hivi.
Ama yaliyomea peke yake bila kupandwa na mtu Mavuno hayo hayana Zaka.
Nayo ni Makapu matano, kwa kauli ya Mtume (saw): (Hakuna katika nafaka wala tende Zaka yoyote mpaka ifike saaq tano) [Imepokewa na Muslim.],
na hii itakuwa ni swaa’(Pishi) mia tatu, nayo ni sawa na (612kg) katika ngano nzuri, na yanachanganywa matunda ya aina moja pamoja ya mwaka mzima ili kukamilisha nisabu; kama sampuli tofautitofauti za tende, kwa mfano tende za sukkari zinachanganywa na tende za barhy, kwasababu ni sampuli za mavuno aina moja, wala haifai kuchanganya aina tofauti ya mavuno kwa nyengine, hivyo basi haifai kuchanganya ngano kwa shayir, wala ngano kwa tende.
Inawajibika utoaji wa Zaka katika nafaka pindi pale zitakapokomaa kuwa tayari, na katika matunda pale yatakapoanza kuonesha uzuri wake, kwa hali ya kwamba yamefikia kuwa mazuri kulika, na atakayeuza matunda au nafaka baada ya wakati wake wa kuwajibika kutolewa Zaka basi Zaka itakuwa ni kwa aliyeuza, kwasababu alikuwa akimiliki mavuno hayo wakati ule wa kuwajibika kutolewa Zaka.
1. Yalazimu kutoa ushuri (10%) Kwa (mavuno) ambayo kwamba hayakunyunyiziwa maji Kwa kuenezewa (na mtu) au kwa kugharamika (kwa mtu), kama vile yaliyonyunyiziwa kwa maji ya mvua au mito.
2. Yalazimu kutoa nusu ushuri (5%) kwa yaliyo nyunyiziwa kwa kuenezwa (na mtu) na kugharamika, kama yale yanayo nyunyiziwa kwa maji ya visima.
3. Yalazimu kutoa rubui tatu ya ushuri (7.5%) kwa yaliyo nyunyiziwa kutumia njia zote mbili, kama vile yanayo nyunyiziwa mara nyengine kwa maji ya mvua na mara nyengine kwa maji ya visima.
Na dalili ni kauli ya Mtume (saw): (Kwa yaliyo nyunyiziwa kwa maji ya mbinguni na mito, na maziwa (yatolewe Zaka) ushuri, na kwa yaliyo nyunyiziwa kwa kutumia saania [ Saania: Ni mnyama anayetumika kunyweshea] (yatolewe Zaka) nusu ushuri) [Imepokewa na Muslim.].
Ni chochote kinachotolewa ndani ya ardhi ambacho kwamba sio sampuli ya ardhi kama vile dhahabu, fedha, vyuma, na vijiwe vya tunu kama vile almasi na rubi, na risasi, na vyenginevyo katika vitu asili vinavyotolewa ndani ya Ardhi.
Ni Mali iliyozikwa ndani ya ardhi kwa kuekwa na mtu, kutokana na dhahabu, na fedha, na mfano wa vitu hivi.
Ni lazima; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: {Enyi mlioamini! Toeni katika vile vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyokutoleeni katika ardhi} (Al-Baqarah: 267),
na kauli ya Mtume (saw): (Na katika hazina iliyozikwa ardhini (toeni) khumusi (1/5)) [Imepokewa na Bukharin a Muslim.].
Hakuna masharti yoyote ya zaka ya hazina iliyozikwa ardhini, basi atakapomiliki mtu hio hazina iliyozikwa ardhini anafaa kutoa zaka yake moja kwa moja.
Ni wajibu mtu kutoa khumusu (1/5) kwa kichache au kingi atakachopata katika madini na hazina iliyozikwa ardhini, kwa jumla ya kauli ya Mtume (saw): (Na katika hazina iliyozikwa ardhini (toeni) khumusi) [Imepokewa na Bukharin a Muslim.].