Sadaka ya kujitolea

11214

 

Maana ya sadaka ya kujitolea

Sadaka ya kujitolea

Ni kinachotolewa kwa lengo la kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni lazima.

Na kwa maana hii inatolewa zawadi na mfano wake kuwa ni katika mambo yanayotolewa kwa lengo la kuzidisha mapenzi, hivyo basi vitu hivi haviingii katika vinavyoitwa sadaka maalumu zilizowekwa na hukumu za sheria.

Hukumu ya sadaka ya kujitolea

Sadaka ya kujitolea ni yenye kupendekezwa kwa wakati wowote ule, na hasaa ikiwa ni wakati unaohitajia kitu, na imehimizwa katika Qur’an na sunnah ya Mtume ﷺ miongoni mwayo ni:

- Maneno ya Mwenyezi Mungu U: {Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili Mwenyezi Mungu Amzidishie mzidisho mwingi} (Al-Baqarah: 245).

- Kutoka kwa Abu Hureirah radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie asema: Amesema Mtume ﷺ: (Atakayetoa sadaka ya tende nzuri alizozichuma kwa kichumo kizuri cha halali – na Mwenyezi Mungu hakubali ila kizuri – hakika Mwenyezi Mungu anakubali sadaka hii kwa Mkono wa kulia, kisha anamkuzia mwenyewe, kama vile anavyokuza mmoja wenu ndama wa farasi wake – mpaka inakuwa mfano wa jabali) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

- Mtume ﷺ amemuhisabu mwenye kuficha sadaka anayotoa miongoni mwa watu saba watakao finikwa na kivuli cha Mwenyezi Mungu, siku ambayo hakuna kivuli isipokua kivuli Chake (Na mtu aliyetoa sadaka akaificha, hata mkono wake wa kushoto usijuwe kilichotolewa na mkono wa kulia) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

- Na kutoka kwa Ka’b Ibn u’jrah radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie kwamba Mtume ﷺ amesema: (Na sadaka zinafuta madhambi kama maji yanavyozima moto) [Imepokewa na Tirmidhi.].

Adabu za sadaka za kujitolea

1. Adabu za lazima

1. Kufanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu U (Ikhlaas) – Anatoa Zaka kwa lengo la kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, sio kwamba aonekane au atajwe vizuri na watu.

2. Kujiepusha na kujisifu (kwamba ni mtoaji) na kuudhi watu (kwa kutoa kwake) kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: { Enyi mlioamini! Msiharibu sadaka zenu kwa masumbulizi na udhia} (Al-Baqarah: 264).

2. Adabu zinazopendekezwa.

1. Inapendekezwa kwa muislamu kutoa sadaka kwa wanaohitajia miongoni mwa jamaa zake ambao sio jukumu lake kuwalisha, kama vile ami zake, na wajomba zakle, na mke kumpa mumewe aliyefakiri, na wengineo, na hivi ni bora kuliko kuwapa sadaka watu wasiokuwa hawa, Anasema Mwenyezi Mungu (s.w): “Yatima aliye jamaa (na asiyekuwa jamaa)” (Al-Balad: 15).

Na katika Hadith: (Hakika ya sadaka kwa masikini ni sadaka, na kwa jamaa yako ni mambo mawili: sadaka na kuunganisha kizazi) [Imepokewa na Nasaai.].

2. Kuchagua katika mali yake mali iliyohalali, nzuri, yanayompendeza nafsiyake. Anasema Mwenyezi Mungu U: {Hamtoweza kuufikia wema (khasa) mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda} (Aali Imran: 92)

3. Kufanya siri katika kuitoa; kwa kuwa hivi ndio karibu zaidi na Ikhlas, na ni mbali sana na kuonesha watu na kutaka kusifiwa, na ni karibu zaidi katika kumkirimu fakiri, Anasema Mwenyezi Mungu U: {Mkizidhihirisha sadaka ni vizuri, na mkizificha mkawapa mafakiri kwa siri basi hivyo ni kheri } (Al-Baqarah: 271).

Na ikiwa katika kuitoa kwa kuonekana kuna maslahi, kama vile watu kuiga kutoa, na kuwatia moyo waliohudhuria, basi inapendekezwa kuitoa wazi, pamoja na kuchunga muislamu niya yake nakuilazimsha juu ya ikhlas

Kutoa sadaka anayoweza hata kama ni kidogo sana, amesema Mtume ﷺ: (Uogopeni moto japo kwa ubali wa tende) [Imepokewa na Bukhari.].

Faida za sadaka za kujitolea

Kwanza: Faida zinazorudi kwa mtu mwenyewe.

1. Kusafisha nafsi, Amesema Mwenyezi Mungu U: { Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (sadaka zao) } (Tawba: 103).

2. Kumuiga Mtume ﷺ, kwani miongoni mwa tabia zake ni utoaji na ukarimu, na alikuwa akitoa sana kiasi cha kuwa haogopi ufukara, na akimwambia Bilal: (Toa ewe Bilal, wala usiogope kwa Mwenye Arshi (Allah SW)kupungukiwa ) [Imepokewa na Al-Bazzar.].

3. Mwenyezi Mungu atamlipa chochote alichokitoa, na atanyanyuliwa daraja mwenye kutoa, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu kwa hili: { Na chochote mtakachotoa, basi Yeye Atakilipa, Naye ni M’bora wa wanaoruzuku} (Saba: 39).

4. Kusafishwa mali kutokana na upuzi wa biashara, kutoka kwa Qays Ibn Abu Gharaza radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie asema: Tulikuwa wakati wa Mtume ﷺ tukijiita madalali [ Samaasira: Madalali Wanakusudiwa wauzaji.]. Mtume ﷺ akatupitia pale tulipokuwa na akatupa jina lililokuwa bora kuliko hilo, akasema: (Enyi wafanyi biashara, hakika uuzaji unafwatiliwa na maneno machafu na viapo, basi changanyisheni [Fashuubuhu: Basi zichanganyeni: Kuamrisha kuchanganyika kwa maana wachanganye mambo yao na utoaji wa sadaka ili iwe kafara ya (kusafisha makosa) kwa Kapitikana baina yao mambo ya uongo na mengineo]. kwa kutoa sadaka) [Imepokewa na Abu Daud.].

5. Kupata malipo mengi, na kusemehewa madhambi kwa kauli yake Mtume ﷺ: “Atakayetoa sadaka ya tende nzuri alizozichuma kwa kichumo kizuri cha halali – na Mwenyezi Mungu hakubali ila kizuri – hakika Mwenyezi Mungu anakubali sadaka hii kwa Mkono wa kulia, kisha anamkuzia mwenyewe, kama vile anavyokuza mmoja wenu ndama wa farasi wake – mpaka inakuwa mfano wa jabali) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

6. Kunufaika Muislamu na sadaka yake ya kuendelea kwa kupata thawabu baada ya kufa. Imepokewa na Abuhureirah radhi za Allah zimfikie kutoka kwa Mtume ﷺ alisema: ( Akifariki mwanaadamu matendo yake yote yanakatika isipokuwa mambo matatu: Sadaka ya kuendelea, au Ilimu yenye manufaa, au Mtoto mwema anaye muombea mzazi wake) [Imepokewa na Muslim.].

7. Kutoa sadaka inazidisha mali na kukuza, na kuonyesha kushukuru kwa mja juu yanema aliyo pewa na Mwenyezi Mungu U na mwenye kushukuru ameahadiwa kuzidishiwa Asema mwenyezi Mungu {Mkishukuru nitawazidishieni } [Ibrahim 07]

Pili: Faida inayorudi kwa jamii.

1. Sadaka inakamilisha ujumbe wa Zaka kwa jamii.

2. Kupatikana kule kutoshelezana na kusaidiana na kupata umakinifu na mapenzi katika jamii ya kiislamu.