Uimamu na Umaamuma

11648

 

Anayestahiki zaidi uimamu

Kwa mpango:

Kwanza: Msomi zaidi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu: naye ni aliyekihifadhi zaidi na kuuzifahamu zaidi hukumu zake.

Pili: Mjuzi zaidi wa Sunna (mafundisho ya Mtume ﷺ: naye ni yule anayejua zaidi ya maana za hadithi zake na hukumu zilizomo ndani ya hizo hadithi.

Tatu: Mwenye kutangulia kugura (Hijra): Mwenye kutangulia kugura kutoka nchi ya kikafiri na kuenda nchi ya kisalmu. Naikiwa Hakuna hijra basi Mwenye kuhama machafu nakurudi kwa Mwenyezi Mungu

Nne: Mkuu zaidi wa miaka: Hapa ni iwapo kuna kulingana katika hayo yaliyopita.

Na dalili ya haya yaliyotangulia ni hadithi iliyopokewa na Ibnu Mas’ud al-Answari t kuwa alisema kwamba Mtume ﷺ alisema: (Atawaongoza watu katika Swala msomi zaidi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Wakiwa wamelingana katika usomi, basi mjuzi zaidi wa Sunna miongoni mwao. Wakiwa wamelingana katika ujuzi wa Sunna ni yule aliyewatangulia katika hijra (kugura), na iwapo wamelingana katika kugura, basi ni yule aliyewatangulia katika Uislamu[ Silman: yaani Uislamu. Na katika riwaya nyingine: “sinnan”]) [Imepokewa na Muslim.].

Na unazingatiwa mpango huu itakikanapo kumuweka imamu wa msikiti au katika jamaa ya watu wasiokuwa na imamu ratibu (naye ni imamu maalumu wa kuswalisha katika msikiti). Ama msikiti ukiwa na imamu ratibu au imamu akawa ni mwenye nyumba, au akawa ni mtawala, [ Takrimah: kile kinachoandaliwa mgeni kukalia.], basi yeye atangulizwa mbele ya mwengine, kwa neno lake Mtume ﷺ: (Na mtu asiwe imamu wa mtu mwingine kwenye mamlaka yake, na aiskaye nyumbani kwake kwenye maandalizi yake isipokuwa kwa ruhusa yake) [Imepokewa na Muslim.].

Kisimamo cha imamu na maamuma katika Swalah

1. Maamuma akiwa mmoja: Sunna ni asimame upande wa kulia wa imamu akiwa amekaribiana naye, kwa hadithi iliyopokewa na Ibnu ‘Abbas  kuwa alisema: (Niliswali pamoja na mtume ﷺ usiku mmoja nikasimama upande wake wa kushoto, na Mtume akashika kichwa changu kwa nyuma yangu akaniweka upande wake wa kulia) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2. Jamaa iwapo ni ya watu wawili na zaidi: Imamu husimama mbele yao kati ya safu, kwa hadithi iliyopokewa na Jabir na Jabaar t kwamba mmoja wao alisimama upande wa kulia wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ na mwingine upande wake wa kushoto. Jabir alisema: (Mtume wa Mwenyezi Munguﷺ akatushika mikono yetu pamoja akatusukuma mpaka akatusimamisha nyuma yake) [Imepokewa na Muslim.].

Kisimamo cha mwanamke

1. Wanaposwali wanawake kwa jamaa, lililo sunna ni asimame imamu wao kati ya safu yao na asiwatangulie.

2. Mwanamke husimama nyuma ya mwanamume iwapo mwanamume ni imamu wake. Na akiswali na wanaume basi atasimama nyuma ya safu.

3. Iwapo wanaume na wanawake wanaswali jamaa, sunna ni wawe nyuma ya wanaume. Na safu zao huwa ni kama safu za wanaume. Abu Hurairah t amepokewa akisema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema: (Bora ya safu za wanawake ni zile zilizo nyuma ya safu, na shari ya safu za wanawake ni zile za mwanzo wake) [Imepokewa na Ibnu Majah.]

Swala ya wanawake
Mwanamke kuwa karibu ya mwanamume

Miongoni mwa hukumu za kumfuata imamu

1. Haisihi kwa mtu aliye nyumbani kwake kumfuata imamu kupitia kusikia sauti yake kwa kipaza sauti au kupitia kusikiliza redio.

2. Inafaa kumfuata imamu kutoka nje ya msikiti iwapo safu zimeungana.

3. Inasihi kwa maamuma kumfuata imamu hata kama wako juu ya sakafu ya msikiti au wakawa chini ya imamu iwapo wanasikia sauti yake.

4. inafaa kwa mwenye kuswali faradhi kumfuata mwenye kuswali sunna au kinyume chake, mfano wa mwenye kuswali swala ya Isha nyuma ya mwenye kuswali Tarawehe, au kuswali pamoja na aliyepitwa na Swala ili apate thawabu ya Swala ya jamaa. Jabir bin Abdillaht amepokewa akisema kwamba Mu’aadh alikuwa akiswali pamoja na Mtume ﷺ kisha akiwajia watu wake akiwaswalisha) [Imepokewa na Bukhari.].

Kufuata kutoka nje ya msikiti

Kumtangulia imamu

1. Amri ya Sheria ni kuwa maamuma amfuate imamu wake kwa kufanya kitendo anachofanya imamu wake papo kwa papo, kwa kauli ya Mtume ﷺ: (Imamu amewekwa afuatwe: akipiga takbri, na nyinyi pigeni takbiri, akirukuu na nyinyi rukuuni na akisujudu, na nyinyi sujuduni) [ Imepokewa na Bukhari na M.uslim.].

2. Imeharamishwa kumtangulia imamu, na Mtume alilitilia hilo makazo mkubwa kwa kusema: (Kwani haogopi mmoja wenu, anapoinua kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu amgeuze kichwa chake akifanye kichwa cha punda au azifanye sura zake kuwa sura za punda) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

3. Mwenye kumtangulia imamu wake kwa kusahau itamlazimu arudi amfuate.

Kuswali nyuma ya asiye na twahara
Swala Haisihi nyuma ya asiye na twahara [ Al-muhdith: ni asye na twahara.]., isipokuwa iwapo hakujulishwa kuwa hana udhu mpaka baada ya kumalizika Swala. Na katika hali hii inasihi swala ya maamuma, na ni juu ya imamu arudie Swala.