Mwanamke Anaweza Kutia Wudhuu Akiwa Katika Hedhi?

SWALI: Asalam Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh Baada ya salam naomba kuuliza kuwa mwanamke anaweza kutia udhu akiwa katika siku zake za hedhi.

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho Hakuna pingamizi lolote kuhusu kuchukua wudhuu ukiwa katika hedhi. Hata hivyo, kuchukua kwako wudhuu hakutakuwa na taathira yoyote kwako hutaweza kufanya ‘Ibaadah zote kwani ‘Ibaadah zinataka utohara. Na utohara wa hedhi ni kuoga mwili mzima sio kuchukua wudhuu. Hata hivyo, ni vyema kuchukua wudhuu kama unataka kwenda kulala kwani hilo ni agizo la Mtume wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa wakati huo kama alivyofanya alipokuwa katika janaba: ((إِذَا أَتَى أَحَدُكُمْ أَهْلَهُ، ثُمَّ أَرادَ أَنْ يَعُودَ فَلْيَتَوَضَّأ ْ(بينهما وضوءاً) ( وفي رواية: وضوءه للصلاة )، فَإِنَّهُ أَنْشَطُ لِلْعَوْدِ)) ((Mmoja wenu anapomjia mkewe kisha akipenda kumrudia mara nyingine, basi achukue wudhuu baina ya nyakati (vitendo) mbili (katika riwaaya nyingine wudhuu ule ule kama wa Swalah) kwani hakika itampa (nashati) uchangamfu kurudia kwake)) [Muslim, Ibn Abi Shaybah na wengineo] Na Allaah Anajua zaidi
Vitambulisho: