Hedhi Haikujitokeza Kikamilifu - Je Swawm Inafaa Siku Hiyo?

SWALI Asalam alykum warahamatu lwah wabarakatu, Swali:- Nilikuwa tanaka kwenda kuswali Adhuhur, kabla ya hapo nilijicheck kwa sababu nilikua nategemea kupata period siku inayoofuata, baada ya kujilazimisha kujicheck kwa mbali sana niliona alama ya mbali ya brown kwenye tissue, nikaacha kuswaali na nikasema ikifika saa tisa nitajicheck tena kama sitoona kitu basi nitaenda kuswali na nilifanya hivyo mpaka nikamaliza kuswali tarawehe sijaona kitu tena na ilipofika usiku saa 8 niliamka kutaka kwenda kuswali sasa nikaona damu. Naomba mnifahamishe vipi swaum yangu kwa siku ile na swala nilizoswali?

JIBU: Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Kwa vile ulikuwa unategemea kuwa siku zako ziko karibu, kisha ukapata damu siku hiyo, basi hiyo siku itahesabika kuwa ni siku ya hedhi. Inavyoelekea ni kuwa haikutoka damu sawa sawa tu, lakini ishara zake tayari zilikuweko. Kwa hiyo itabidi uilipe siku hiyo na Swalah ikiwa umeziswali basi huna la kufanya, kwani mwanamke hatakiwi kulipa Swalah ila anatakiwa alipe Swawm pekee. Tafadhali bonyeza hapa pia utapata FATWA inayojibu swali kama hilo: Matone Ya Damu Ya Hedhi Kabla Damu Kutoka Na Allah Anajua zaidi




Vitambulisho: