Vyombo

Vyombo

 • Maelezo kuhusu Vyombo
 • Kutumia vyombo vya dhahabu na fedha
 • Kutumia vyombo vilivyolihimiwa kwafedha

 • Maelezo kuhusu Vyombo

  Vyombo

  Vyombo vya kuhifadhia maji na vinginevyo

  Kutumia vyombo vya dhahabu na fedha

  1. katika kula na kunywa

  Ni haramu kuvitumia kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Msinywe kwenye vyombo vya dhahabu na fedha, na msile kwenye sahani zake. Kwani hivyo ni vyao wao ulimwenguni na ni vyetu kesho Akhera) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

  Na kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Yule anayekunywa kwenye chombo cha fedha, kwa hakika anaingiza tumboni mwake moto wa Jahanamu) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

  2. Kutumia vyombo vya dhahabu na fedha kwa matumizi yasiyokuwa ya kula na kunywa

  Inafaa kuvitumia kwa matumizi mengine yasiyokuwa kula na kunywa, kama kutawadhia na mengineo kwa hadithi ilio tangulia kuwa imekaza kuvitumia kwa ajili ya kula na kunywa, na imethubu kwa hadithi ya Ummu Salamah t alikuwa na chombo (juljul) la fedha ambayo ndani yake kulikuwa na baadhi ya nywele za mtume ﷺ.

  Kula kenye chombo cha dhahabu
  Kula kwenye chombo cha fedha

  Kutumia vyombo vilivyolihimiwa kwafedha

  Inafaa kutumia vyombo vilivyolihimiwa kwa fedha kidogo kuwapo na haja, kwa kuwa imethubutu kwamba kopo la Mtume ﷺ lilivunjika akapafunga pale palipopasuka kwa silsila ya fedha. [Imepokewa na Bukhari].

  Birika ya fedha kwa ajili ya kutawadhia
  Kutumia chombo kilcholihimiwa kwa fedha
  Uvaaji dhahabu kwa wanaume
  Haifai kwa mwanamume kuvaa dhahabu, kwa hadithi iliyothubutu kutoka kwa Abu Musa al-Ash›ari kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema: (Limeharimishwa vazi la hariri na dhahabu kwa wanaume wa umma wangu na limehalalishwa kwa wanawake wao) [Imepokewa na Tirmidhi].


Tags:


)