Nyakati (mawaaqiit)

Nyakati (mawaaqiit)

 • Maana ya miiqaat
 • Aina ya nyakati

 • Maana ya miiqaat

  Nyakati kilugha

  Kuweka mpaka baina ya vitu viwili.

  Nyakati kiistilahi ya sheria

  Ni mipaka iliyowekwa na sharia kwa ajili ya ibada na yawakati na Namahali.

  Aina ya nyakati

  Kwanza: Nyakati za mahali

  Nyakati za mahali

  Ni sehemu zilizowekwa na Sheria kuhirimia kutoka hapo

  Haifai kwa anyetaka kuhiji au kufanya Umra azipite sehemu hizo isipokuwa awe amehirimia. Nazo ni sehemu tano [Al-Mawaaqiit wa Ab›aaduhaa. Sheikh Abdullah Al-Bassaam, Gazeti la Majma’ al-Fiqh al- Islaami, Idadi: 3, Juzu: 3, ukurasa 1553]:

  1. Dhul Hulaifah

  Nayo ipo upande wa kusini wa mji wa Mtume wa Madina, na unaitwa «Abyaar ‹Ali». Iko mbali na Makka kwa masafa ya kilimita 420.

  Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Madina.

  Dhul Hulaifah

  2. Juhfah:

  Nayo iko karibu ya mji wa Raabigh, na ina umbali wa kiasi cha kilomita 186 kutoka Makka.

  Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Shaam, Masri na nchi za upande wa maghribi

  Juhfah

  3. Yalamlam:

  Nayo ni bonde kubwa kwenye njia ya watu wa Yaman kwenda Makka.

  Kwasasa inaitwa: Assa›diyyah, na iko mbali na Makka kwa kiasi cha kilomita 120.

  Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Yaman.

  Yalamlam

  4. Qarnul Manaazil:

  Na sasa inaitwa ( Assaylul Kabiir), na iko mbali na Makka kwa kiasi cha kilomita 75.

  Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Najd na Twaif. Na juu yake, kwenye njia ya Twaif upande wa Hadaa kuna mahali panapoitwa Waadii Muharram.

  Na pote pawili ni sehemu ya kuhirimia watu wa Najd na wale wanaokuja kupitia njia ya Twaif.

  Qarnul Manaazil

  5. Dhaatu ‹Irq:

  na sasa inaitwa ( Dhariibah au Khuraibaat).

  Napo ni mahali upande wa Mashariki ya Makka. Umbali wake na Makka ni kiasi cha kilomita 100. Na kwa sasa hapo mahali pamehamwa.

  Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa upande wa Mashariki (Iraki, Irani na nchi za nyuma yake. Na dalili ya yaliyopita ni ni riwaya iliyopokewa kutoka kwa Ibnu Abbas t kuwa alisema: (Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliwawekea watu wa Madina Dhulhulaifah iwe ni mahali pa wao kuhirimia, akawawekea watu wa Sham hapo Juhfa. Akawawekea watu wa Najd hapo Qarnulmanaazil, Akawawekea watu wa Yaman hapo Qarnulmanaazil na akasema: ”Sehemu hizo ni zao wao na wanaokuja hapo kati wa watu wa maeneo mengine wanaotaka kuhiji au kufanya Umra”) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

  Ama Dhaatu ‘Irq haikutajwa kwenye hadithi iliyotangulia, na lililowekwa ni ‘Umar ibnu l- Khattaab [Imepokewa na Bukhari.].

  Dhaatu ‹Irq
  Maelezo

  - Mwenye kuvuka sehemu hizi za mikati bila ya kuhirimia ni lazima kurudi na kuhirimia ikiwezakana, na isipoweza kufanya hivyo basi atawajibika kutoa fidiya, nao ni mbuzi atakae mchinja makka na agawanye nyama yake kwa masikini wa makka.

  - Mwenye kupita sehemu za Mikaati kwa mtu asie kuwa ni wasehemu hiyo basi atahirimi hapo, lau mtu wakutoka najdi amekuja kwa njia ya watu wa madina atahirimia sehemu ya watu wa madina (Abyaar Ali)

  - Mtu ikiwa nymba yake iko ndani ya sehemu ya kuhirimia kwa upande wa makka basi Mtu huyu atahirimia hija na umra sehemu alipo Mfano wa watu wa Jiddah na Bahra na Ashraa’i.

  - Mwenye kuja kwa njia ya anga na bara, na bahari, huyu atahirimia akiwamkabala na sehemu ya Mikati iliyo karibu. Kwa kauli ya umar binl-khatwab (angaliyani mkabala wake kutoka kwenye njia yenu) [Imepokewa na Bukhari.]

  - Mwenye kutia nia ya kuhiji kwa mtu wa makka au asie kuwa mtu wa makka huyu atahirimia makka, ama akitaka kufanya Umra atatoka kwenda tan’iim na Ji’iraan nazo ni sehemu ziko nje ya mipaka ya haram

  Pili: Nyakati za kuhirimia

  Nyakati za kuhirimia

  Zama za kuhiji na kufanya Umra

  A. Nyakati za Hijja

  Ni miezi ya Hija nayo ni: Mfungomosi, Mfungopili na siku kumi za Mfungotatu.

  B. Nyakati za Umra

  Ni mwaka mzimaTags:


)